LYRIC

[Verse 1]

Mi Kwako Sikuingia Miguu
Mikono Hadi Kichwa Kiufupi Mazima
Nikiaminii
Wakufa Kuzikana
Yani Hoi Sio Nafuu
Mahututi Kabisa Hata Mashaka Sina
Nikiaminii Tutatengwa Na Maulana
Mvumilivu Ula Mbivu
Nimengoja Mpaka Zikaoza
Naambulia Maumivu
Ingali Sina Wa Kunipoza
Sijui Yangu Stahamilivu
Kunyenyekea Kwaniponza
Napambania Utulivu
Mwenzangu Chuki Unaikoza
Sikukufuta tu Machozi
Ulipolia Nlilia Na Wewe
Sa Mbona Wanilipa Majonzi
Yani Stress Mapombe Nilewe
We Ndio Wangu Yesu Mkombozi
Sa Mbona Petro Unaniacha Mwenyewe
Nikose Usingizi Na Njozi
Ndio Ufurahi? Okey sawa!
Si Unataka Nitukanwe..!

[Chorus]

Ongeza Ongeza Bado (Nidhalilike)
Ongeza Ongeza Bado (Nikose Pakuificha Sura)
Ongeza Ongeza Bado (Marafiki Wanicheke, Waning’ong’e Adaa)
Ongeza Ongeza Bado

[Verse 2]

Mmh!
Kisicho Kuua Ukukomaza eti Kiuaskari
Huo Msemo Mi Nakataa
Maana Jua Linapo Angaza Ndio Sina Afadhali
Mie Kwangu Ni Mabalaa
Ooh Ooh! Najitahidi Kumsinga Mwali
Ila Somo Ananikataa
Ooh Ooh! Penzi Letu Sie La Kibatari
Anayamwaga Mafuta Ya Taa
Kutwa Ni Vurugu Ndani
Purukushani Apakaliki
Roho Inaniuma Yani
Kwanini Sa Tunagombana Sweet
Ooh Ooh! Jema Gani
Niambie Labda Nitеnde Kipi
Ata pakucheka Honey
Eti Utani Unapaniki
Naеlewa!
Ridhiki Mafungu Saba Na La Kwangu Sita
Naelewa!
Sikutoshi Labda Kukuridhisha
Sikukufuta Tu Machozi (Sii iih iih)
Ulipolia Nililia Na Wewe (Nawewe!)
Sa Mbona Wanilipa Majonzi
Yani Stress Mapombe Nilewe
We Ndio Wangu Yesu Mkombozi
Sa Mbona Petro Unaniacha Mwenyewe
Nikose Usingizi Na Njozi
Ndio Ufurahi? Okey Sawa!
Si Unataka Nitukanwe..!

[Chorous]

Ongeza Ongeza Bado (Eeh Eeh Eeh! Nidhalilike)
Ongeza Ongeza Bado (Eeh! Nikose Pakuificha Sura)
Ongeza Ongeza Bado (Ndugu Jamaa Wanicheke, Waning’ong’e Adaah!)
Ongeza Ongeza Bado (Aah Nikose pakuificha sura…!)
Aah Waning’ong’e Adaah!

 

GET AUDIO HERE


Added by

Mp3juice

SHARE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

VIDEO